FluxPro.artCreate

podcast style sitting in chair and saying about these things in swahili PODCAST: "KUSHINDA SI KUNG'ANG'ANIA KILA KITU" Watu wengi wamelelewa na sentensi, "Winners never quit." Lakini watu wengi hawaelewi maana yake. Ukweli ni huu: Mshindi si yule asiyewahi kuacha. Mshindi ni yule anayejua nini anapaswa kuacha na nini anapaswa kuendelea kupigania. Kuna tofauti kubwa kati ya kuvumilia na kung'ang'ania. Ukiona unaendelea kuweka muda, nguvu na pesa kwenye kitu ambacho kila siku kinakurudisha nyuma, hiyo siyo grit tena. Hiyo ni ego. Watu wenye akili wanajua kitu kinaitwa sunk cost fallacy. Kwa lugha ya mtaani, ni ile hali ya kusema, "Nimeshafika mbali sana, siwezi kuacha sasa," wakati ukweli ni kwamba kila siku unazidi kupoteza. Hebu fikiria mfano huu. Mtu ana biashara ambayo imekuwa ikipata hasara kwa miaka miwili. Badala ya kukubali imefeli, anaendelea kukopa pesa, kuuza mali zake na kuomba ndugu wamchangie. Mwisho wa siku anafilisika kabisa. Mwingine, baada ya kuona data na hali halisi, anafunga biashara mapema. Anachukua alichojifunza, anaanza biashara nyingine yenye nafasi nzuri zaidi, na baada ya mwaka mmoja anatengeneza faida kubwa. Sasa jiulize, mshindi ni nani? Yule aliyeng'ang'ania mpaka akaanguka, au yule aliyekubali kuachia mapema ili ashinde vita vingine? Kujua wakati wa kuacha si udhaifu. Ni intelligence. Ni strategy. Hata kwenye mahusiano, kazi, biashara au ndoto, si kila vita ni vya kupigana mpaka mwisho. Vingine vinakuja kukufundisha tu, si kukaa navyo milele. Kumbuka hii: Winners don't quit their future. They quit what is destroying it. Kwa hiyo usiogope kuachia kitu ambacho hakikupi tena thamani. Kwa sababu mara nyingi, kitu unachokishikilia ndiyo kinazuia nafasi ya kitu bora kuingia. Wakati mwingine, ushindi haupatikani kwa kushikilia. Unapatikana kwa kuachia.

20
0
Safe
Guidance 1
Seed 729242051234453
Steps 9
Public
Input Images

More from Chenga Chenga

Explore more work from this creator.

View more from Chenga Chenga